Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania

"Inaunganisha Tanzania na Dunia"
ISO Imethibitishwa 9001:2015; 14001:2015 & 45001:2018

Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Abiria wote wanaowasili nchini wakitoka nje ya nchi, wanalazimika kisheria kufuata taratibu za forodha, mathalani i.e., upekuzi na kufanya tamko la forodha kwa bidhaa/vitu vyenye thamani.



Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea www.tra.go.tz kuhudu ushuru na forodha.

​​​​​​Unaweza kusubiria abiria wanaowasili nje au ndani ya Kiwanja cha Ndege ikitegemea na hali ya chenyewe Kiwanja na utashi wako.

Taarifa za miruko ya ndege zinaweza kupatikana kwa kufuata maelekezo yafuatayo: -




  • Tafadhali, tembelea www.taa.go.tz ili kupata taarifa za ndege zinazoondoka na zinazowasili (FIDS),

  • Angalia luninga zenye taarifa ya miruko ya ndege zilizopo maeneo tofauti tofauti katika viwanja vyetu vyote vya ndege.

  • Uliza katika madawati yetu ya maelezo yaliyoko katika viwanja vyetu vya ndege.

Ni abiria tu wenye bodi za kupandia ndege husika na nyaraka zinginezo za kusafiria, ndiyo pekee wanaruhusiwa kufika vyumba vya kuondokea au vyumba vya kuunganishia ndege.



Kwa maelezo zaidi, tuandikie barua pepe kupitia info@airports.co.tz.