Dhumuni kuu la Mkataba wa Huduma kwa Wateja ni kuongeza ufahamu kuhusu uwepo na ubora wa huduma zitolewazo na TAA. Utawasaidia wateja wetu kufahamu haki na wajibu wao na jinsi ya kutoa mrejesho pale wanapoona kushuka kwa viwango vya huduma zetu kama ilivyoainishwa katika Mkataba huu.
Hivyo, Mkataba unatafasiri dira, dhima, falsafa, maadili pamoja na utamaduni, mila, desturi, kanuni za maadili (codes of conduct), kipimo na tathmini ya huduma zetu kwa wateja, ikiwa ni pamoja na kufanya marekebisho pale panapohitajika.
Aidha, Mkataba huu ni chombo cha uwazi, kwani unatoa uwazi wa huduma zitolewazo na mamlaka, viwango na ubora unaotakiwa. Kwa kushirikiana pamoja na wateja na wadau wetu, tumeweza kuweka viwango vya ubora wa huduma vinavyokidhi matarajio ya wateja, na kuwafanya watumishi wahakikishe wanawahudumia wateja kwa nidhamu na ueledi ili kuongeza tija na uzalishaji.
Mkataka huu wa Wateja utasaidia pia kutathmini ubora wa huduma zitolewazo na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), na jinsi ya kuwasilisha mrejesho utakaosaidia kufanya maboresho pale patakapohitajika.
Unaweza kuisoma na kupakua mkataba wa huduma kwa wateja Mkataba huduma kwa mteja