DIRA
Kuwa mtoaji bora wa huduma za (uendeshaji) viwanja vya ndege duniani.
DHIMA
Kutoa huduma bora na uwezeshaji katika viwanja vya ndege kwa kuzingatia usalama na ufanisi kwa wadau wa Viwanja vya Ndege na nia ya kukuza uchumi na maendeleo ya jamii.
MAADILI MAKUU
Uadilifu
Ubunifu
Uwajibikaji
Kuwajali Wateja
Kufanya kazi kwa weledi
Kufanya kazi kwa pamoja
Ulinzi na Usalama Viwanjani
MAJUKUMU
1. Kupanga, kuandaa na kutekeleza mipango kwa ajili ya ujenzi, uendelezaji, uendeshaji, usimamizi na utunzaji wa miundombinu, majengo na vifaa vya viwanja vya ndege vya Serikali;
2. Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Serikali na umma kuhusu masuala ya kitaifa na kimataifa kuhusu uanzishwaji, uendelezaji, usimamizi, uendeshaji na utunzaji wa viwanja vya ndege;
3. Kutoa vifaa muhimu vya viwanja vya ndege, huduma za ulinzi na usalama na huduma nyingine zinazohusiana na hizo kwa ajili ya kuwezesha ndege, abiria, mizigo na vifurushikwa viwanja vya ndege vya Serikali;
4. Kusimamia shughuli za kila siku za viwanja vya ndege vya Serikali kwa kuzingatia kanuni na viwango;
5. Kuhakikisha huduma za zimamoto na uokoaji zinatolewa katika viwanja vya ndege vya Serikali;
6. Kutunza ardhi za viwanja vya ndege na kufuatilia ujenzi na uwekaji wa vizuizi katika maeneo ya karibu na viwanja vya ndege vya Serikali;
7. Kusimamia utunzaji na uhifadhi wa bidhaa hatarishi ndani ya viwanja vya ndege vya Serikali;
8. Kushughulikia dharura zinazohusu masuala ya uendeshaji ndani ya viwanja vya ndege vya Serikali na maeneo ya jirani;
9. Kuvitangaza viwanja vya ndege vya Serikali, kuvutia mashirika ya ndege na kuibua fursa za kibiashara;
10. Kuweka na kutunza vifaa vya kisasa vya teknolojia ya habari na mawasiliano ili kuimarisha shughuli za viwanja vya ndege vya Serikali;
11. Kuanzisha taasisi za mafunzo kwa ajili ya mafunzo ya usimamizi wa viwanja vya ndege na karakana kwa ajili ya matengenezo ya vifaa na mitambo ya Mamlaka;
12. Kutoa huduma za ushauri elekezi kuhusu uendelezaji na usimamizi wa viwanja vya ndege ndani au nje ya nchi; na
13. Kutekeleza majukumu mengine ambayo yanaweza kutolewa kwa Mamlaka na Sheria hii au sheria nyingine yoyote.