Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania

"Inaunganisha Tanzania na Dunia"
ISO Imethibitishwa 9001:2015; 14001:2015 & 45001:2018

Msaada

Mizigo

Mizigo iliyokusudiwa kuingia ndani ya ndege haipaswi kuwa na urefu zaidi ya inchi 22 na upana inchi 14 na kimo inchi 9 (hii ikiwa ni pamoja na mkono wa kuvutia na matairi). Pamoja na kwamba hakuna kiwango cha mwisho cha uzito, inashauriwa uzito usizidi kilo 10. 

Aidha, vimiminika viwe chini ya mililita 100, na endapo vitafikia mililita 100 au zaidi basi vihifadhiwe kwenye mizigo itakayopakiwa chini. Abiria wanashauriwa wasihifadhi mali za thamani kubwa mathalani fedha, vito, kompyuta mpakato, kamera na aina hiyo kwenye mizigo inayohifadhiwa chini.

Ukaguzi wa Ndege

Kwa ndege za kimataifa, abiria anatakiwa kuanza ukaguzi saa tatu (3) kabla ya muda wa ndege kuondoka; na kwa ndege za ndani ya nchi, abiria anatakuwa kuanza ukaguzi saa mbili (2) kabla ya muda wa ndege kuondoka.

Wakati, kwa ndege za kimataifa, ukaguzi husitishwa/hukoma saa moja (1) kabla ya muda wa ndege kuondoka; na kwa ndege za ndani ya nchi ukaguzi husitishwa dakika arobaini na tano (45) kabla ya muda wa ndege kuondoka. Abiria wanaotumia viwanja vyetu vya ndege wanashauriwa kusoma kwa umakini taarifa zilizoambatanishwa kwenye tiketi zao.

Ukaguzi wa Kiusalama:

Abiria wanashauriwa kutokusafiri ndani ya ndege na vitu hatarishi, mathalani vifaa vya mionzi, vimiminika vinavyoweza kulipuka gesi iliyokandamizwa (CNG) kwani vitu hivi vinaweza kuhatarisha usalama wa ndege. 

Endapo ungependa kusafiri na vitu hivi, unashauriwa kuwasiliana na wakala wako wa usafiri kwa msaada zaidi.

Forodha

Abiria wote wanaowasili kutoka nje ya nchi na wenye mizigo, wanalazimika kufanyiwa ukaguzi na kufuata taratibu za tamko la forodha kwa bidhaa/vitu vyenye thamani kubwa. 

Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea www.tra.go.tz kuhudu ushuru na forodha.

  • Uingizaji wa Bundiki na Risasi: Abiria wanatakiwa kupata kibali kutoka Idara ya Polisi kabla na mapema.
  • Uingizaji wa Wanyama na Mimea: Kabla ya kupanda ndege, abiria wanatakiwa kuwasiliana na wakala husika katika viwanja vyetu vya ndege wanapowasili au wanapokuwa wanaondoka.

Uhamiaji:

Abiria wote wa wanaowasili kutoka nje ya nchi, wanatakiwa:

  • Kujitokeza binafsi mbele ya Afisa wa Uhamiaji wakiwa wamejaza na kusaini Kadi ya Tamko la kuwasili;
  • Kuwasilisha kwa Afisa wa Uhamiaji Pasi za kusafiria au nyaraka nyingine ya kusafiria iliyo idhishwa;
  • Kwa abiria kutoka nje (foreigners) watatakiwa kuonesha Viza au kuwasilisha ombi la viza wanapowasili. Na kwa wale wageni wanaoishi nchini kuonesha Kibali cha Makazi (Residence Permit/Pass); kuonesha tiketi ya kurudi walikotoka au Ushahidi wa kuonesha wanaendelea na safari nchi zingine; pamoja na kuonesha uthibitisho wa kifedha unatosheleza kipindi chote wakiwa nchini Tanzania. 

Kwa taarifa zaidi tafadhali tembelea www.immigration.go.tz.