Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) inaelewa na kuamini kwamba mafanikio yake yanatokana na uwajibikaji wa kurejesha sehemu ya faida kwa jamii kwa kuzingatia umuhimu na uendelevu. Dhamira ya TAA inaunga mkono juhudi za Mamlaka kuwekeza kwa jamii na kuboresha maisha ya watanzania kupitia mipango/programs ya kuondoa umaskini na kuleta maendeleo ya kiuchumi.
TAA imedhamiria kudumisha na kuimarisha utamaduni wa utawala bora unaozingatia uwajibikaji kwa jamii na mazingira katika uendeshaji shughuli zake huku ikiweka mizania sawa kati ya uzalishaji faida na ustawi wa jamii.
TAA inatambua kuna uwezekano wa matukio au dharura/majanga yanayoweza kujitokeza na kupelekea madhara yasiyokusudiwa wakati ikitekeleza majukumu yake ya msingi wakati wa uendelezaji na uendeshaji wa shughuli za viwanja vya ndege nchini. Kwa kuzingatia aina ya kazi zake, madhara ya awali ni ya kimazingira na jamii zilizokaribu na viwanja vya ndege. Hivyo, matamanio na mikakati yetu katika utekelezaji wa CRS ni kuzijengea uwezo na kuzijengea fursa jamii duni zilizo jirani na viwanja vyetu ili kuzijengea mazingira rafiki kwa ustawi wa jamii na ukuaji kiuchumi.