Karibu
Karibu katika Tovuti Rasmi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)!
Ni heshima na furaha yangu kuwaalika wageni wetu wote: wanaosafiri na wasafiri watarajiwa katika tovuti yetu!
Katika tovuti hii, utagundua taarifa muhimu, zana nyeti za kimtandao, pamoja na sasisho (updates) kuhusu taasisi yetu: utekelezaji wa majukumu yake katika kuhakikisha ufanisi wa usafiri kwa ndege ndani na nje ya nchi yetu; wakati huo huo tukiwezesha ukuaji wa sekta nyeti katika uchumi wan chi yetu.
Ukiwa wewe ni mdau wetu wa muda mrefu, mshirika mtarajiwa au mdau unayevutiwa na shughuli zetu; tunakukaribisha kwa moyo mkunjufu kuwasiliana nasi kupitia tovuti hii.
Asante kwa kutuunga mkono na kwa kuchagua viwanja vyetu vya ndege kuwa lango lako kuelekea sehemu zingine ulimwenguni.