Kiwanja cha Ndege Musoma
Kiwanja cha ndege cha Musoma ni moja kati ya viwanja vya ndege 59 vya serikali vilivyopo chini ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania. Kiwanja kina eneo lenye ukubwa wa Hekari 103.1 sawa na mita za mraba 505,232.3 kikihudumu kama Kiwanja kikuu katika Mkoa wa Mara na Mkoa wa Jirani Simiyu. Kilianzishwa mwaka 1950 kabla ya Uhuru kikiwa ni kiwanja kidogo (airstrip) kinachomilikiwa na Kanisa na baadae kumilikiwa na Serikali ya Tanganyika wakati huo. Kiwanja kipo daraja la 1C (Aerodrome Category 1C) ICAO Code HTMU, IATA code MUZ na daraja la 1 kwa upande wa zimamoto (fire Category I) na kinafanya kazi masaa 12 (mawio na machweo). Kiwanja kipo katika mwinuko wa mita 3,783m kutoka usawa wa bahari na wastani wa nyuzi joto 25.40 0C. Kiwanja hiki kwa sasa hakina ndege ya ratiba kinatoa huduma kwa ndege zisizo na ratiba (non-scheduled flights) na pia kama lango la kuingia na kutoka kwa ndege/abiria wanaotoka/kwenda nchi za Jirani (Kenya, Uganda, Rwanda n.k) wanaozuru mbuga yetu ya Serengeti na maeneo mengine katika mikoa hii miwili.
Mashirika ya ndege yanayotoa huduma katika kiwanja cha ndege Musoma; Coastal Aviation, Auric Air, Grumet, Regional Air, Z. Boscovic, Arusha Medical, Safari Plus, AMREF, Frankfurt Zoological Society, Air Kenya, Northern Air, TANAPA, East African Air, Ndege za Serikali