Kiwanja hiki kipo katika Ukanda wa Utalii karibu na Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara, hivyo kiwanja hiki ni kiunganishi cha watalii kutoka mataifa mbalimbali kuelekea Hifadhi
za Taifa; Ziwa Manyara, Serengeti, Tarangire, Ngorongoro na maeneo mengine ya utalii. Kiwanja cha Lake Manyara kipo 03o22’31.6”S na 035o49’04.84”E katika kitongoji cha
Sangaryani, kijiji cha Kilimamoja, kata ya Rhotia, Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha na umbali wa takriban kilomita 150 kutoka Jiji la Arusha na kilomita 25 kutoka Halmashauri
ya Wilaya ya Karatu. Uwanja wa ndege uko futi 4150 juu ya usawa wa bahari na wastani wa nyuzi joto 24°C.
Kiwanja kina uwezo wa kuhudumia ndege za ukubwa wa (aina ya Cessna caravan 208) na DHC 6. Eneo la Maegesho ya ndege (Apron) lina uwezo wa kupaki ndege aina ya
Cessna Caravan 13 kwa wakati mmoja.
Kiwanja cha ndege cha Lake Manyara kinafanya kazi masaa kumi na mbili kwa siku zote saba za wiki (12/7) kuanzia machweo hadi mawio.
Barabara ya Kuruka na Kutua Ndege “Runway” 12/30 : Ina urefu wa mita 1220 na Upana 21m
Eneo la Maegesho ya Ndege “Apron”: Ina ukubwa wa 980.1sqm , ina uwezo wa kupaki ndege 13 zenye ukubwa aina ya cessina caravan kwa wakati mmoja
Jengo la Abiria: Eneo la Jengo lina ukubwa wa 404 sqm ,katika jengo la abiria ukumbi wa wageni wanaoondoka unauwezo wa kuhudumia wageni 60 kwa pamoja, ukumbi wa wageni wanaowasili unauwezo wa kuhudumia wageni 30 kwa pamoja na ukumbi wa wageni mashuhuri unauwezo wa kuhudumia wageni 12 kwa pamoja.
Mashirika ya ndege yanayotoa huduma
Kiwanja kinatoa huduma kwa ndege zisizokuwa na ratiba maalumu. Hivi sasa tuna mashirika ya ndege ya Auric air, Coastal Travel ltd, Air excel , Regional Air services,
Zantas Air, Safari Plus ltd, Grumeti Air, Flight link, Tropical Air, Jambo Aviation, Air Eclipse, Shine Aviation, Arusha Medivac, Tanzanair, Crop Cair Aviation, Flying Zanzibar, TANAPA, JWTZ, Air Kenya, Amref (Flying Doctors).