Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania

"Your Gateway to Global Horizons"
ISO Imethibitishwa 9001:2015; 14001:2015 & 45001:2018

Kiwanja Cha Ndege


Picha za Viwanja Vya Ndege
Taarifa za Viwanja vya Ndege

Kiwanja cha Ndege Kigoma

Kiwanja cha Ndege Kigoma(ICAO: HTKA, IATA: HKQ)  ni moja kati ya viwanja vya ndege vinanyosimamiwa, kuendelezwa na kuendeshwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA). Kiwanja hiki kipo kwenye kundi la pili, daraja la 3C(Aerodrome Category), kikiwa na daraja la 5 la viwango vya huduma za Zimamoto na Uokoaji (Fire Cat 5). na kina Leseni uendeshaji mpaka tarehe 30/3/2025. Kiwanja hiki kinahudumia wasafiri wa ndani ya nchi na wakati mwingine kinahudumia wasafari wa kimataifa hasa nchi ya Burundi.

Kiwanja cha ndege Kigoma kilianzishwa mwaka 1954 kwa lengo la kusaidia safari za viongozi wa serikali magharibi mwa Tanganyika.

Mnamo mwaka 1979 ukarabati mkubwa na mdogo ulifanyika kwa nyakati tofauti ili kukiboresha kiwanja kwa ajili ya kuwezesha Ndege kutoka mashirika ya ndege ya Afrika mashariki kutumia kiwanja hiki.

Mnamo mwaka 1981 maboresho makubwa yalifanyika, maboresho haya yalihusisha upanuzi wa jengo la abiria na jengo la utawala.

Mnamo mwaka 2010 maboresho makubwa yalifanyika ambayo yalilenga kuboresha barabara ya Ndege mpaka urefu wa 1800m na upana wa 45m na njia unganishi mbili (taxway) A na B zenye urefu wa 150m na upana wa 18m.

Kiwanja kinafanya kazi kila siku kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa kumi na mbili na nusu jioni (sunrise and sunset). Kiwanja cha ndege kigoma kipo 5.5km kazikazini-mashariki mwa mji wa kigoma kikiwa na eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 1,989,534.

Kwa sasa kiwanja cha Ndege Kigoma kina kampuni moja tu (ATCL) inayotoa huduma kwa Ndege yenye ratiba. Ndege kubwa inayotua kiwanja cha Ndege Kigoma ni Bombadier DH8 Q400 yenye uwezo wa kubeba abiria 76 pamoja na wahudumu. Ndege hiyo inafanya kazi siku zote saba kwa wiki na kwa siku tatu hufanya kazi kama Ndege ya kimataifa yaani kutoka Kigoma kwenda Burudi na kutoka Burundi kuja Kigoma.

Pia kiwanja cha ndege Kigoma kinatoa huduma kwa Ndege zisizo na ratiba yaani “adhok”.