Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania

"Inaunganisha Tanzania na Dunia"
ISO Imethibitishwa 9001:2015; 14001:2015 & 45001:2018

Kiwanja Cha Ndege


Picha za Viwanja Vya Ndege
Taarifa za Viwanja vya Ndege

Kiwanja cha Ndege Arusha

Kiwanja cha Ndege Arusha ni miongoni mwa viwanja vya ndege 59 vinavyosimamiwa, kuboreshwa na kuendeshwa chini ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kiwanja hiki kipo katika kundi la II. Kiwanja cha ndege hiki kinafanya miruko ya ndege ya ndani ya Nchi pekee. Kiwanja kinapatikana upande wa magharibi mwa jiji la Arusha , takribani kilomita 7 au (4NM) kutoka katikati ya Jiji la Arusha. Kiwanja wa ndege uko futi 4567 juu ya usawa wa bahari wenye wastani wa nyuzi joto 23ᵒC.

HISTORIA

Kiwanja cha ndege cha Arusha kilijengwa mwaka 1956 na Kanali Gray ambaye alikuwa mkulima mkubwa wa kilimo cha kahawa na mtama katika eneo la Burka na Mateves , Baada ya uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 Kiwanja hichokilichukuliwa rasmi na Serikali.

Kiwanja cha ndege kiliendeshwa chini ya mashirika ya ndege ya Afrika Mashariki, baada ya kuvunjika kwa jumuiya ya Afrika Mashariki 1977 kiwanja kilikabidhiwa kwa idara ya Kilimo inayoitwa KILIMO HANGER kwa ajili ya shughuli za unywiziaji dawa kudhibiti wadudu waharibifu wa mazao.

Kiwanja cha ndege cha Arusha kinasimamiwa na Meneja wa Kiwanja ambaye pia ana jukumu la kusimamia Kiwanja cha kidogo cha ndege cha Loliondo.

Kulingana na viwango vya ICAO, kiambatisho cha 14 Kiwanjacha ndege cha Arusha kimeainishwa ni kiwanja cha ndege daraja la 3C.

Kwa sasa kiwanja kina njia ya kuruka na kutua ndege yenye urefu wa mita 1860 na upana wa mita 30 ikiwa na mwelekeo wa 09 na 27, PCN 15/F/B/Y/T baada ya kukamilika kwa upanuzi wa mradi wa barabara ya kurukia na kutua ndege ambao una jumla ya urefu wa mita 1860 na sehemu za kugeukia ndege kila upande.

Kiwanja cha ndege cha Arusha kina maungio matano (5) ya barabara za ndege (taxi ways)  A, B, C, D na P na eneo la maegesho mawili (2) ambayo ni;

(i) Eneo kuu la maegesho ya ndege lenye ukubwa wa mita za mraba 15,000 ambalo lina uwezo wa kuegesha ndege tatu (3) aina ya ATR 72 au Bombardier Dash 8 Q400 pamoja na ndege ndogo aina ya C208 kumi na tano kwa mara moja.

(ii) Maegesho ya pembezoni yenye ukubwa wa mita za mraba 8,925 yenye uwezo wa kuegesha ndege zenye uzito chini ya tani 12  kumi na tano(15) aina ya C208.

Kiwanja cha ndege cha Arusha kina jengo la abiria lenye uwezo wa kuhudumia abiria 1000 kwa wakati mmoja.

MASAA YA UENDESHAJI 

Kiwanja cha ndege cha Arusha kinafanya kazi masaa kumi na mbili (12) kuanzia machweo hadi mawio.

HUDUMA YA UOKOAJI NA ZIMAMOTO (RFFS)

Kitengo cha zima moto daraja namba tano (5) kwa mujibu wa madaraja ya zimamoto ya viwanja vya ndege vya shirika la usimammizi  wa ndege duniani (ICAO), kituo kina vifaa vyote muhimu kwa uokoaji ikiwa ni pamoja na gari la zimamoto lenye uwezo wa kubeba maji lita 6500 na madawa ya kuzimia moto lita 650, vifaa vya mawasiliano, kemikali za moto na vifaa vingine vya uokoaji.