Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania

"Your Gateway to Global Horizons"
ISO Imethibitishwa 9001:2015; 14001:2015 & 45001:2018

Habari

UKARABATI NA UPANUZI WA KIWANJA WA NDEGE TABORA WAFIKIA 97% ️


image title here


Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya Shilingi Bilioni 24.6 kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Tabora, kazi inayotekelezwa na M/s Beijing Construction Engineering Group Co. Ltd (BCEG).

Kazi zinazofanywa katika mradi huu ni pamoja na:
Ujenzi wa jengo la abiria lenye uwezo wa kuhudumia abiria 240 kwa wakati mmoja,
Maegesho ya magari na barabara ya kuingia na kutoka kiwanjani,
Uzio wa ndani kwa ajili ya usalama
Maduka ya biashara, Mfumo wa uratibu wa usimamizi wa mizigo, Kituo cha hali ya hewa na Jengo la kuongozea ndege.

Kukamilika kwa Mradi kutakuwa na Faida mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kukuza fursa za uwekezaji na biashara,
Kurahisisha usafiri wa anga katika Kanda ya Magharibi, Kuchochea uchumi wa mkoa wa Tabora na Kukuza utalii na kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.

Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu ya usafiri wa anga kwa maendeleo ya taifa.