Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania

"Inaunganisha Tanzania na Dunia"
ISO Imethibitishwa 9001:2015; 14001:2015 & 45001:2018

Habari

TAA kuhakikisha kanuni na taratibu zote zilizowekwa zinafuatwa ili kulinda usalama katika viwanja vya ndege nchini.


image title here


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Abdul Mombokaleo amesema watahakikisha kanuni na taratibu zote zilizowekwa zinafuatwa ili kulinda usalama katika viwanja vya ndege nchini.
Mombokaleo ametoa kauli hiyo mkoani Dar es Salaam wakati akifunga maadhimisho ya Wiki ya Usalama wa Anga, hafla iliyofanyika katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Amesema kutokana na kuwepo kwa vitisho vya vitendo vya kigaidi katika maeneo mbalimbali duniani, ni lazima kuwe na mbinu bora za usafirishaji ambazo pia zitasaidia kuboresha hali ya usalama katika viwanja vya ndege nchini.
Mombokaleo amesema viwanja vya ndege lazima viwe na usalama kwani havipo kwa kwa ajili ya huduma za usafiri pekee bali pia ni kwa ajili ya biashara kutokana na kuwa ni vyanzo vya mapato kwa Taifa.
Amesisitiza kuwa katika usafiri wa anga usalama ndio jambo la msingi, hivyo kila mtu anapaswa kuwa na utamaduni wa kuhakikisha usalama huo unakuwepo kwa ajili ya faida ya sasa na kwa kizazi kijacho.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya Wiki ya Usalama wa Anga kwa mwaka huu ni 'Usalama wa anga ni jukumu la kila mtu'.