Shirika la Ndege la Afika ya Kusini (South African Airways) limerejesha rasmi safari zake za Afrika Kusini – Tanzania na Tanzania Afrika ya kusini ikiwa ni miaka takribani mitano kupita toka Shirika hilo lisitishe safari zake nchini mwaka 2020.
Safari hizo zimeanza rasmi mara baada ya kutua usiku wa tarehe 21 Januari, 2025 katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere na kupokelewa na aliekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Bw. Salim Msangi,pamoja na Balozi wa Afrika Kusini Nchini Tanzania Noluthando Mayende Malepe pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TAA Bw. Abdul Mombokaleo aliembatana na menejimenti ya TAA.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Bw, Msangi amesema tukio la kurejesha safari kwa ndege hiyo ni kielelezo cha wazi cha kuendelea kimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kibiashara kati ya Tanzania na Afrika kusini huku akieleza juhudi kubwa zinazofanywa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kujenga na kuimarisha uchumi wa nchi haswa katika sekta ya usafiri wa anga.
Aidha Balozi wa Afrika Kusini nchini Noluthando Mayende Malepe amesema “Nimefurahishwa sana na ndege yetu ya South African Airways kurejea tena Tanzania kwani sisi ni ndugu na marafiki wa kihistoria na pia wanachama wa Jumuiya ya umoja wa Africa (AU) na jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC).
Naye Mkurugenzi wa wa Shirika la ndege la South Africa Aiways Prof, John Lomola amesema ni furaha sana kwa mara nyingine kutua katika hii ardhi nzuri ya Tanzania ndege hii itafanya safari zake mara saba kwa wiki kutoka kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha O.R Tambo cha nchini Afrika ya Kusini kuja Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Awali akizungumza wakati wa Hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TAA Bw. Abdul Mombokaleo amewashukuru wadau wote wa viwanja vya ndege na sekta ya usafiri wa anga kwani wamekuwa chachu katika kuiwezesha TAA kuendelea kufanya vizuri zaidi katika kutimiza majukumu yake huku akiamini namna walivyoweza kuchangia kutengeza mazingira ambayo yanawezesha hata mashirika ya ndege kuendelea kuja nchini.
Pamoja na hayo ameeleza kuwa kurejea kwa Shirika la ndege la Afrika ya Kusini kunaongeza idadi ya mashirika ya ndege kufikia 24 yenye miruko ya moja kwa moja kutoka Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere