SHILINGI BILIONI 73.5 KUJENGA MIUNDOMBINU YA KISASA KATIKA KIWANJA CHA NDEGE MTWARA.
Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa serikali inaendelea kuboresha na kujenga viwanja vya ndege ili viwanja hivyo viweze kutoa huduma za usiku na Mchana na viwe vya kisasa ,
Mbarawa ameyasema hayo kwenya hafla ya utiaji Saini ya Mkataba wa usanifu na ujenzi wa jengo la Abiria, Vituo vya Zimamoto na Hali ya Hewa, Pamoja na Mnara wa kuongozea ndege katika kiwanja cha ndege cha Mtwara wenye thamani ya shilingi bilioni 73.5.
“Serikali inaendelea kujenga na kuboresha viwanja vya ndege hapa nchini viwanja hivyo ni kiwanja cha ndege cha Musoma, Iringa, Songwe , Msalato na kiwanja cha ndege cha Mtwara ili viwanja hivyo viwe vya kisasa” Amesema Mbarawa.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Selemani Kakoso ameutaka uongozi wa wizara ya Uchukuzi kuhakikisha inamsimamia mkandarasi huyo ili akamailishe ujenzi huo kwa wakati .
“Kamati ya Bunge ya Miundombinu inaipongeza serikali kwa hatua hii, pia ni jambo jema kwa TAA kusimamia ujenzi huo kwani umeweka vitu vyote vinavyohitajika hivyo Wizara hakikisheni mnamsimamia Mkandarasi ili akamilishe kazi hii kwa wakati, Alisema Kakoso.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania Bw, Mussa Mbura amesema kuwa jengo hilo litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni moja kwa mwaka na 500 kwa mara moja ikiwa mkataba huo utachukua miezi 36.
Mkataba huo umeingiwa na Serikali kupitia Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania (TAA) na kampuni ya China Railway Construction Engineering Group(CRCEG )kutoka nchi ya China.