Serikali imesema takriban sh. Bilioni 37 zimetumaka kwaajili ya ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya Kiwanja cha ndege cha Songea hatua ambayo itachagiza kuongezeka kwa safari za ndege ambazo zitakidhi soko la wasafiri wa anga wa mkoa wa Ruvuma.
Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa alipofanya ziara ya kukagua maboresho yaliyofanyika kwenye kiwanja hiko, ambapo amesema maboresho hayo ni chachu itakayosaidia safari za ndege kufanyka kila siku za wiki.
“Kukamilika kwa uwanja wa ndege huu kumesababisha shirika letu la ndege kuanza safari zake za kawaida Air Tanzania sasa inakuja mara 3 kwa wiki tulitamani ije mara nyingi baadaa ya mara tatu labda tufanye ianze kufanya mara tano kwa wiki lakini baadae ianze kuja kila siku” Alisema Mbarawa
Pamoja na hilo Waziri Mbarawa amesema kwa sasa wananchi wataendelea kutumia jengo dogo la abiria wakati Serikali inaendelea kufanya mchakato wa ujenzi wa jengo la kisasa la abiria ambalo litaweza kutoa huduma bora kwa wananchi ambazo zitaendana na hadhi ya kiwanja hiko.
“Eneo ambalo bado tunalifanyia kazi ni jengo la abiria kwa hadhi ya kiwanja hiki tunatakiwa tupate jengo la abiria ambalo ni jengo la kisasa ambalo linaweza kutoa huduma bora kabisa kwa wananchi wetu hapa tunalojengo dogo ambalo tunalifanyia marekebisho ambalo litakua jengo la muda huku tunafanya mpango ya kujenga jingo jingine “Alisema Mbarawa
Kwa niaba ya wananchi mkuu wa mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema anaishukuru Serikali kupitia wizara ya uchukuzi kwa kuimarisha sekta ya uchukuzi mkoani humo na kuendelea kutoa kipaumbele kwenye utekelezaji wa miradi iliyochini ya wizara hiyo.
“Niendelee kukushukuru kwa jinsi ulivyokua karibu na mkoa huu kuakikisha sekta nyingi ambazo zipo chini ya wizara yako unazipa upendeleo na jicho la karibu” alisema
Kwa upande wake Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Songea Mhandisi Danstan Komba amesema Miundombinu iliyoboreshwa imeleta matokeo chanya baada ya safari za ndege kuongozeka kutoka abiria 3000 kwa mwaka kabla ya mwaka 2021 hadi kuhudumia abiria 19300 kwa mwaka.
“Kabla ya mwaka 2021 tulikua tunahudumia ndege takribani 3000 kwa mwaka lakini baada ya maboresho hayo kuanzia novomba 2021 wakati Air taznania ilipoanza tena safari yake mkoani Ruvuma sasa tunauwezo wa kuhudumia abiria 19300 hayo ni maendeleo makubwa kwa mkoa wetu” alisema Mhandisi Komba.
Akizungumzia maeneo yaliyoboresha ni pamoja na njia ya kutua na kurukia ndege ambayo mwanzo ilikua na urefu wa mita 1600 na sasa inaurefu wa mita 1860 hivyo kufanya utuaji wa ndege kuwa wa salama na rafiki zaidi
Aidha amesema serikali imefanya maboresho mkubwa kwenye eneo la usalama kwa maana ya run way, usimikaji wa taa za kuongozea ndege kwa ajili ya kuwezesha ndege kufanya safari za usiku lakini pia wakati wa mchana ambapo kunakua na ukungu mzito,
Maboresho mengoine ni pamoja na kituo cha kupokea nishati kwa maana ya maji na umeme, katika line ya umeme yenye msongo wa kilowatt 33 na lami ambayo inakidhi viwango na vigezo na yenye miundombinu toshelevu kwaajili ya utuaji wa ndege.