Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania

"Inaunganisha Tanzania na Dunia"
ISO Imethibitishwa 9001:2015; 14001:2015 & 45001:2018

Habari

SERIKALI YATENGA SHILINGI BILIONI 29 KWA AJILI YA UKAMIlLSHWAJI JENGO LA ABIRIA UWANJA WA NDEGE MWANZA


image title here


Waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa Makame Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania kubuni uendeshaji wa viwanja hivyo kibiashara ili viweze kuleta tija ya kiuchumi.

Rai hiyo ameitoa Jijini Mwanza wakati wa hafla ya utiaji saini kati ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania ( TAA ) na Mkandarasi wa kukamilisha ujenzi wa Jengo la Abiria katika kiwanja cha  Ndege mkoani Mwanza ambao utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 29.

Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka vya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mussa Mbura amesema, Serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 29 kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la abiria  katika uwanja huo kwa kufanya kazi zifuatazo,

Ukamilishaji wa maeneo ya biashara nje ya jengo, ujenzi wa maegesho ya magari mia tatu, ujenzi wa barabara ya kuingia na kutoka kwenge jengo la abiria, ujenzi wa barabara kiunganishi kati ya jengo hilo na maegesho ya ndege na ujenzi wa uzio wa usalama kuzunguka jengo lote.

Mbunge wa Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza Tabasam Hamis akishuhudia utiaji wa saini ujenzi wa jengo hilo, amemuomba  mkandarasi wa ujenzi huo kuutekeleza usiku na mchana ili uweze kutoa huduma haraka ndani ya kipindi cha miezi michache.

 Aidha Tabasam amesema pamoja na fursa ya ujenzi huo anamuomba Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuboresha Barabara ya Mwanza - Lamadi iweze kupanuliwa ili iendane na upanuzi wa uwanja huo na usafirishaji wa wageni kutoka ndani na nje ya nchi   ufanyike kwa wepesi zaidi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Selemani Kàkoso amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Daraja la JPM,Meli ya Mv Mwanza Hapa kazi tu na miradi mingine ya kimkakati.

Pia Kakoso  ameitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania kuendelea kusimamia viwanja hivyo nchini kutokana na baadhi ya viwanja kujengwa na Wakala ya Barabara Tanzania  ( TANROADS ) na vikijengwa bila udhibiti unaotakiwa kama ilivyoelekezwa.