Naibu Waziri Wa Uchukuzi David Kihenzile ametoa wito kwa watumishi wa Taasisi za Wizara kutumia vyema fursa waliyopewa katika utumishi wa Umma ili utumishi wao uwe na matokeo chanya.
Akizungumza jijini Tanga mara baada ya kutembelea na kupokea taarifa ya utendaji wa Kiwanja Ndege cha Tanga, Naibu Waziri Kihenzile amesema mafanikio yanayopatikana kupitia utendaji kazı yanategemea weledi,ubunifu na kujituma kwa watumishi hao.
Naibu Waziri Kihenzile ametumia nafasi hiyo kuzipongeza taasisi za Wizara zinazofanya kazi kiwanjani kwa kuhakikisha huduma zinazotolewa zinaendelea kuvutia mashirika ya Ndege kuendelea kutumia Kiwanja hicho.
Aidha, Naibu Waziri Kihenzile amesema pamoja na Serikali kuendelea kununua Ndege pia Sekta Binafsi inaweza kuendelea kuwekeza kwenye usafiri wa anga ili kukidhi mahitaji ya soko la usafiri huo.
Kwa upande wake Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Tanga Yusufu Zuberi Sood ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya maboresho ya Miundombinu Nchini hali inayochochea ukuaji wa usafiri wa anga Nchini.