Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania

"Your Gateway to Global Horizons"
ISO Imethibitishwa 9001:2015; 14001:2015 & 45001:2018

Habari

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Bw. Abdul Mombokaleo ametembelea Kiwanja cha ndege cha Morogoro


image title here


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Bw. Abdul Mombokaleo ametembelea Kiwanja cha ndege cha Morogoro kwa ajili ya ukaguzi wa miundombinu ya kiwanja pamoja na kuzungumza na watumishi kiwanjani hapo.
Katika ziara hiyo Mkurugenzi Mkuu ameambatana na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Bi. Irene Minja ambapo wamekutana na watumishi kiwanjani hapo na kusisitiza juu ya utendaji kazi kwa kuzingatia weledi.
Hata hivyo amesisitiza watumishi hao kuwa na ushirikiano na Sekta Binafsi haswa ikizingatiwa kiwanja hicho kina Uwekezaji wa Kampuni ya Kuunganisha ndege ya Airplane Africa Limited ikiwa ni azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan juu ya ushirikishwaji wa Sekta binafsi katika kuleta maendeleo ya Taifa.
Pamoja na mambo mengine katika ziara hiyo Bw. Mombokaleo alitembelea kampuni ya kuunganisha ndege ya Airplane Africa Limited na kujadili masuala mbalimbali ya kibishara ili kuendelea kukuza Sekta ya Usafiri wa Anga Nchini.