Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania

"Inaunganisha Tanzania na Dunia"
ISO Imethibitishwa 9001:2015; 14001:2015 & 45001:2018

Habari

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka afanya mkutano na wafanyakazi wa Makao Makuu


image title here


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Bw, Abdul Mombokaleo leo tarehe 18 Septemba,2024 amefanya mkutano na wafanyakazi wa Makao Makuu kwa lengo la kufahamiana na kuweka mikakati zaidi ya kujenga taasisi kwa maslahi mapana ya nchi.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Transit uliopo katika jengo la 1 la abiria katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
“Tumekutana katika kikao hiki kwa mara ya kwanza kwa lengo la kufahamiana na kujadili njia bora zaidi za kuendelea kutekeleza ipasavyo majukumu yetu ya msingi katika kuendeleza, kuboresha na kuendesha viwanja vya ndege nchini ”amesema Bw Mombokaleo.
Pamoja na hayo ameahidi kufanyia kazi yale yote ambayo yameelezwa na baadhi ya watumishi kwa ajili ya uboreshaji wa utendaji kazi ili kuzidi kuipeleka taasisi mbele zaidi.