Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imetunukiwa tuzo kutokana na Tanzania kuwa moja kati ya nchi zenye viwanja vya ndege vyenye ubora wa usalama duniani.
Tuzo hiyo imetolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Tathimini za Huduma na Ubora wa huduma katika nyanja ya usafiri wa anga (ACI).
Akipokea tuzo hiyo Jijini Johannesburg, Afrika ya Kusini kwa niaba ya TAA, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Profesa Godius Kahyarara amesema tuzo hiyo inaonesha dhamira ya dhati ya Serikali katika kusimamia kwa viwango vya juu usalama wa abiria katika anga la Tanzania.