Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania imeibuka kwa kuwa Mshindi namba moja na kupewa tuzo ya uchangiaji wa kipekee katika Mkutano wa 17 wa tathmini ya Utendaji kazi kwa Taasisi za Wizara ya Uchukuzi zilizofanya vizuri kiutendaji. Tuzo hiyo imetolewa leo tarehe 25 Octoba 2024 na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile na kupokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri Bw.Juma Hassan Fimbo wakati wa kuhitimimisha mkutano huo katika kituo cha mikutano (AICC) Jijini Arusha.