Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania

"Your Gateway to Global Horizons"
ISO Imethibitishwa 9001:2015; 14001:2015 & 45001:2018

Habari

KIBAHA SEKONDARI YAADHIMISHA MAHAFALI YA 58 KWA MAFANIKIO MAKUBWA


image title here


Shule ya Sekondari Kibaha imeadhimisha mahafali yake  58 ya Kidato cha Sita kwa mafanikio makubwa ya kitaaluma na kijamii. Hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya shule, ilihudhuriwa na wageni mbalimbali, wazazi, walimu na wanafunzi. Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Abdul Mombokaleo ambaye alitoa hotuba yenye hamasa kwa wahitimu na jamii nzima ya shule.

Katika hotuba yake, Mkurugenzi Mkuu aliwahimiza wahitimu kutumia elimu waliyoipata kama chombo cha mabadiliko chanya katika jamii na taifa kwa ujumla. Aliwataka kuipenda Tanzania, kuwa wajasiri kwa kupambana na maisha, kuwa wapatanishi kwa kuwa sauti ya utulivu, kuwa wakarimu, wenye shukrani na kutokuisahau shule yao ya kibaha. Pia alisisitiza umuhimu wa nidhamu, maadili mema, na kutumia teknolojia kwa manufaa ya maendeleo yao.

Katika hotuba yake, Mkuu wa shule, Mwalimu George Marriot Kazi, alitoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha elimu na miundombinu kwa ujenzi wa mabweni mawili, madarasa mawili, na matundu ya vyoo 10 kwa thamani ya zaidi ya Tsh milioni 300.

Pia alimpongeza mgeni rasmi kwa mchango wake mkubwa katika kuwezesha Uwekezaji kwenye TEHAMA, ambapo shule imepata madarasa janja, kompyuta, na intaneti ya bure kwa mwaka mzima

Mkuu wa shule alieleza mafanikio ya shule katika ufaulu wa kitaifa, michezo na nidhamu. Ambapo Kwa mwaka 2024, wanafunzi wote wa kidato cha nne walifaulu kwa daraja la kwanza, huku 98% ya watahiniwa wa Kidato cha Sita wakipata daraja la kwanza na waliobaki daraja la pili ikiwa ni Wastani wa ufaulu wa alama A kwa shule ikiwa ni kiwango cha juu zaidi kitaifa.

Shule ya Sekondari Kibaha, iliyo chini ya Shirika la Elimu Kibaha, imeendelea kuwa chimbuko la viongozi mbalimbali wa kitaifa, akiwemo Rais wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, pamoja na viongozi wengine waandamizi serikalini na taasisi binafsi.

Mahafali hayo yaliambatana na burudani mbalimbali kutoka kwa wanafunzi, zikiwemo nyimbo,mashairi na maigizo yaliyobeba ujumbe wa kitaaluma na kijamii.