Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania

"Inaunganisha Tanzania na Dunia"
ISO Imethibitishwa 9001:2015; 14001:2015 & 45001:2018

Maendeleo Ya Viwanja Vya Ndege

Maeneo
Ukarabati na Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege Kigoma.

Mradi wa Upanuzi wa Ukarabati wa Kiwanja unahusisha maeneo (scope of works) yafuatayo:-

  1. Ujenzi wa jengo la abiria(Terminal Building) lenye mita za mraba 7700,lenye uwezo wa kuhudumia abiria 400,000 kwa mwaka.
    1. Upanuzi wa maegesho ya ndege kutoka mita za mraba 14,000 hadi mita za mraba 40,000 yenye uwezo wa kupaki ndege kubwa 3 aina ya B737,
    2. Ujenzi wa mnara wa kuongozea ndege(Control Tower)
    3. Ujenzi wa barabara za kuingia kiwanjani(Access Roads) zenye urefu wa 1.2km,
    4. Ujenzi wa maegesho ya magari (Car parking) yenye uwezo wa kuegesha magari zaidi ya 100 kwa wakati mmoja,
    5. Usimikaji wa mifumo ya taa za kuongozea ndege (Airfield Ground Lighting Systems)
    6. Ujenzi wa kituo kidogo cha umeme(Electrical Power sub-station)
    7. Ujenzi wa uzio wa usalama wenye urefu wa 7.5km.
  2. Mradi huu wa ukarabati na Upanuzi wa kiwanja cha Ndege Kigoma ukikamilika utakuwa na  manufaa yafuatayo;

Kuongezeka kwa ndege za abiria na mizigo,

Kuimarisha usafiri wa anga katika Ukanda wa Magharibi na nchi jirani,

Kuchochea shughuli mbalimbali za ukuaji wa kiuchumi na kijamii.

Kuongezeka kwa fursa za kibiashara katika Mkoa wetu wa Kigoma na mikoa jirani.

Kuimarisha na kuendeleza utalii

Taarifa za urekebishaji

Bei : TZS. 46,683,370,304.39 Tsh

Hali : OnProgress

Mfadhili : European Investment Bank (EIB)

Mahali : Kigoma Airport

Muda : 18 Months