Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania

"Inaunganisha Tanzania na Dunia"
ISO Imethibitishwa 9001:2015; 14001:2015 & 45001:2018

Wasifu

Ndugu Mussa I. Mbura
Ndugu Mussa I. Mbura
Mkurugenzi Mkuu

Mamlakaya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) iliundwa tarehe 29 Novemba, 1999 ikiwa ni sehemu ya programu ya uboreshaji wa Utumishi wa Umma ambao pamoja na mambo mengine ulikusudia kupunguza gharama kwa Serikali, kuongeza ubora katika utendaji na ufanisi katika utoaji Huduma kwa Umma. TAA ilianzishwa kupitia Tangazo la Serikali Na. 404 la Mwaka 1999 chini ya Kifungu cha 3 cha Sheria ya Wakala wa Serikali Sura Na. 245 ya mwaka 1997 na ilizinduliwa rasmi tarehe 3 Disemba, 1999. TAA ilianzishwa ili kusimamia, kuendesha na kuendeleza viwanja vya ndege vya Serikali isipokuwa vilivyo chini ya Mamlaka za Hifadhi, Halmashauri, Jeshi, n.k vilivyopo Tanzania Bara.