Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Mussa Mbura amekutana na Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Uganda (UCAA), ambao umetembelea Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania na kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kwa lengo la kujifunza namna Viwanja vya Ndege vinavyoendeshwa na kubadilishana uzoefu wa masuala ya uendeshaji wa viwanja vya ndege katika nchi za jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Aprili 27, 20 kwenye ukumbi wa watu mashuhuri (VIP II) uliopo katika jengo la pili la abiria, kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere. Mkurugenzi Mkuu (TAA) aliwashukuru wajumbe wa bodi hiyo kuja na kukichagua kiwanja cha ndege JNIA kujifunza namna Viwanja vya Ndege Tanzania vinavyoendeshwa na huu umekuwa ushirikiano bora kati ya Tanzania na Uganda katika maswala ya usafiri wa Anga.
Akiongea kwa niaba ya wajumbe, Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhe. Jaji. Dkt Steven B. K. Kavuma alieleza namna walivyofurahishwa na ziara hiyo na kwamba wamejifunza mengi katika shunguli zinazohusu uendeshaji wa Viwanja vya NdegeMsafara wa ujumbe huo ulikuwa na wajumbe 11 ukiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Jaji. Dkt Kavuma na Mkurugenzi Mkuu wa UCAA Bw. Fred Bamwesigye.
Categories
Corporate Events 3Recent News