Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Juma Hassan Fimbo, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Abdul Mombokaleo, wamesaini mkataba wa utekelezaji na utendaji kazi kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Hafla ya kusaini mkataba huo imefanyika leo katika Makao Makuu ya Mamlaka, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa kila mwaka unaolenga kuimarisha uwajibikaji, kuongeza ufanisi wa kiutendaji na kuhakikisha utekelezaji wa malengo ya taasisi ndani na nje ya TAA.
Kupitia mkataba huu, menejimenti na Bodi zinajipanga kwa pamoja kuhakikisha huduma bora, uwajibikaji wa hali ya juu na matokeo chanya kwa wadau wote wa sekta ya usafiri wa anga nchini.