Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania

"Your Gateway to Global Horizons"
ISO Imethibitishwa 9001:2015; 14001:2015 & 45001:2018

Habari

KIHENZILE:KIWANJA CHA NDEGE CHA SUMBAWANGA NI FURSA KWA MAENDELEO YA UCHUMI NA KIJAMI


image title here


Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga kinatarajiwa kuchochea maendeleo ya Uchumi na kijamii katika mkoa wa Rukwa, mikoa ya jirani na nchi kwa ujumla kutokana na kurahisisha shughuli mbalimbali za usafiri na usafishaji, biashara, kilimo sanjari na utalii.
Akizungumza leo, 24 Aprili, 2026 kwenye hafla ya uzinduzi wa Uendeshaji wa Kiwanja hicho, N/Waziri Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile amesema uwepo wa Kiwanja hicho ni fursa kwa wananchi wa mkoa huo na mikoa ya jirani kujiinua kiuchumi kupitia fursa mbalimbali zinazotokana na uwepo wa Kiwanja hicho.

“Wananchi wa Sumbawanga, nitoe wito kwenu kulinda miundombinu ya Kiwanja, hii ni fursa ya kipekee kwenu, pia nitoe wito kutumia fursa hii ya uwepo wa Kiwanja hiki kwa manufaa, tumieni kujiinua kiuchumi,” amesema Mhe. Kihenzile.

Aidha, Mhe. Kihenzile ameipongeza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, kwa jitihada zake za kusimamia ipasavyo Viwanja vya ndege nchini, ikiwemo kusimamia kwa wakati maboresho ya kiwanja cha Sumbawanga,
Hata hivyo Mhe; Kihenzile ameitaka ATCL kuharakisha taratibu ili angalau mwezi Mei 2026 kuanza safari katika kiwanja hicho angalau mara mbili kwa wiki.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini, Mhe. Aeshi Hilaly amewaasa wananchi wa Sumbawanga kulinda na kutunza miundombinu ya Kiwanja hicho cha Ndege ili kuendelea kulinda rasilimali za umma.

Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Abdul Mombokaleo amesema ukarabati na upanuzi wa Kiwanja hicho ulianza Septemba 2023 ambapo jitihada zilifanyika kuhakikisha Kiwanja kinakamilika kwa wakati. Ujenzi wa mradi huo ulihusisha Jengo la Abiria, njia ya kuruka na kutua Ndege, Mifumo ya Taa, Maegesho ya Ndege na Ujenzi wa uzio wa usalama.

“Kukamilika kwa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga kunarahisisha shughuli mbalimbali za usafiri na usafirishaji sanjari na kuchochea ukuaji wa Uchumi wa Rukwa na mikoa ya jirani kupitia Vivutio mbalimbali vya Utalii na Milima ya Ufipa,” amesema Bw. Mombokaleo.