IMG_3760.JPG

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhandisi, Dk. Charles Tizeba alipowasili kwenye jengo la mkandarasi, BCEG anayefanya upanuzi na ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Mwanza hivi karibuni. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, Dk. Anthony Diallo na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ilemela, Amina Masenza.

IMG_3760.JPG

Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege vya Mikoani (DRA), Mhandisi Thomas Haule akisoma taarifa ya maendeleo ya mradi wa upanuzi na ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Mwanza kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

IMG_3760.JPG

Mkuu wa wilaya ya Ilemela, Amina Masenza (kushoto) akiwa na Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza, Easter Madale wakimsubiri Waziri Mkuu, Mizengo Pinda awasili kwenye eneo la ujenzi wa jengo la kuongozea ndege.

IMG_3760.JPG

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto) na Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege vya Mikoa (DRA), Mhandisi Thomas Haule alipokagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la kuongozea ndege katika kiwanja cha Ndege cha Mwanza karibuni.

IMG_3760.JPG

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitafakari jambo baada ya kuoneshwa maendeleo ya urefushaji barabara ya kuruka na kutua ndege katika kiwanja cha Ndege cha Mwanza unavyoendelea wakati akiwa juu kilimani linakojengwa jengo la kuongozea ndege.

IMG_3760.JPG

Moja ya mitambo ya kuchakata kokoto kwa ajili ya kuchanganya lami za kujengea barabara ya kutua na kuruka ndege kwenye kiwanja cha ndege cha Mwanza iliyosimikwa na mkandarasi, BCEG.

IMG_3760.JPG

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na baadhi ya wahandisi wa kampuni ya BCEG, mkandarasi anayefanya upanuzi na ukarabati wa miundombinu ya kiwanja cha ndege cha Mwanza alipokagua jengo la kuongozea ndege kilimani. Anayeangalia kamera(tai nyekundu) ni Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege vya Mikoa (DRA), Mhandisi Thomas Haule na anayeangalia juu ya jengo ni Mhandisi Geoffrey Asulumenye).

IMG_3760.JPG

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiangalia kutoka juu, kilimani linakojengwa jengo la kuongozea ndege, maendeleo ya urefushaji wa njia ya kutua na kuruka ndege kwenye kiwanja cha ndege cha Mwanza. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhandisi, Dk. Charles Tizeba.

IMG_3760.JPG

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na vibarua wa kampuni ya ukandarasi ya BCEG ya China inayopanua na kukarabati kiwanja cha ndege cha Mwanza baada ya kukagua eneo ambalo njia ya kutua na kuruka ndege limerefushwa kwa mita 500 zaidi. Wa pili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo, Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza, Easter Madale na kulia mwisho ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Godfrey Lutego.