• Waziri wa Ujenzi, Uchuzi na Mawasiliano akisikiliza taarifa ya maendeleo ya mradi kutoka kwa msimamizi wa Ujenzi Bw, Hank katika eneo la “check in” alipotembelea Jengo la tatu la abiria mapema leo. Kulia baada ya Waziri ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania Bw, Richard Mayongela.

 • Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akisikiliza jambo kutoka kwa afisa wa kampuni ya mafuta PUMA Bw, Mohamed Ngayaika, alipotembelea kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere leo. (Kulia ni Bw. Richard Mayongela).Kaimu Mkurugenzi Mkuu TAA.

 • Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano) Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akisikiliza jambo kutoka kwa Mkurugenzi wa uendeshaji TanzanAir Bw. Abdul Kadir Mohamed (alienyoosha mkono) alipotembelea ofisi hizo zilizopo ndani ya Kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere (JNIA) . Kushoto ni Bw. Richard Mayongela Kaimu MKurugenzi Mkuu viwanja vya ndege Tanzania.

 • Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA) BW, Richard Mayongela (Aliyesimama mbele) akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali. Kushoto mbele ni Mhe: Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye.

 • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald kuashiria ufunguzi rasmi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera.

 • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald mara baada ya ufunguzi.

 • Mhandisi Balton Komba wa Tanroads (wan ne kushoto) akimpa maelezo ya jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kushoto), na Wakwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela.

 • Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege vya Mikoa (DRA), Bw. Valentine Kadeha (katikati) akishirikiana kupanda mti na wanafunzi wa shule ya Mpakani ya Mabibo, katika maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, iliyoadhimishwa jana kwa wafanyakazi wa taasisi mbalimbali wa Sekta ya Uchukuzi kufanya usafi nje ya Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) na Soko la Mabibo.

 • Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dr. Leonard Chamuriho akipanda mti ndani ya Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT), ikiwa ni moja ya kazi zilizofanyika jana kwenye kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, iliadhimishwa kwa kufanyika usafi maeneo ya nje ya chuo hicho na soko la Mabibo.

 • Mojawapo wa Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Swalha R. Soka akishiriki zoezi la upandaji miti ndani ya Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT)

Kamati ya Bunge Yapongeza Serikali kwa Ujenzi TB III

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeipongezaSerikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kwa kujenga jengo zuri la tatu la abiria (TB III) litakaloboresha zaidi huduma za usafiri wa anga.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Profesa Norman Sigalla (Makete) wakati Wajumbe wa Kamati hiyo walipotembelea jengo hilo katika ziara yao ya kukagua miradi ya Serikali mwanzoni mwa wiki.

Jengo hilo linajengwa katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kwa Euro milioni 254 (sh. Bilioni 560) za mkopo kutoka Benki ya HSBC ya Uingereza na CRDB kwa dhamana ya Serikali ya Tanzania na Uholanzi.

Tayari TAA imeshamlipa Mkandarasi wake, Bam International ya Uholanzi, Euro milioni 96 baada ya kukamilisha asilimia 60 ya kazi. Jengo hilo linajengwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ipo katika hatua za mwisho.

Mwenyekiti Sigalla na Wajumbe wengine wa Kamati hiyo walieleza kuridhishwa na kazi nzuri iliyofanywa na Serikali kujenga jengo hilo linalotarajiwa kukamilika Desemba 2017.

Baada ya kufurahishwa na kazi hiyo nzuri na kushauri uboreshaji zaidi wa utendaji, wabunge waliahidi kuisukuma Serikali iiwezeshe zaidi TAA kifedha ikamilishe miradi yake kwa wakati.

Walisema hayo baada ya kupokea taarifa za utendaji na miradi ya TAA kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi George Sambali na Mkurugenzi anayesimamia Mradi wa TB III, Mhandisi Mohammed Millanga.

Pia walipokea taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha aliyeeleza uhaba wa fedha wanazopewa unavyowaathiri katika kuendesha shughuli nyingi za kiwanja hicho ambacho ni kitovu cha mapato ya TAA.

TAA inayosimamia viwanja 58 vya ndege vya Serikali Tanzania Bara, hukusanya zaidi ya sh. Bilioni 67 lakini hupewa sh. Bilioni 17 tu kwa ajili ya kujiendesha huku JNIA ikipata sh. Milioni 700 tu kwa mwezi ukitoa za mishahara.

Taarifa za watendaji TAA zilionesha maendeleo ya miradi ya ujenzi wa miundombinu ya viwanja vya ndege inayoendeshwa na kusimamiwa na TAA, jengo la TB III, ukarabati JNIA, changamoto zake kubwa na mipango ya Serikali kuzitatua.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi Sambali alieleza dhamira ya TAA kuwa na kiwanja kipya cha ndege nje ya Dar es Salaam au kupanua JNIA kwa kuongeza njia zaidi za kurukia ndege ifikapo 2030.

Hata hivyo, aliwaeleza wabunge changamoto ya TAA kutekeleza dhamira hiyo kuwa ni ulipaji fidia kwa wananchi na reli ya TAZARA kupanua eneo la sasa la JNIA au kupata zaidi ya dola milioni 500 kuanzisha kiwanja kipya nje ya Dar es Salaam.

Wabunge waliitaka TAA kufanya tathmini ya gharama za upanuzi wa JNIA kwa kulipa fidia wananchi na kuhamisha reli ya Tazara au kujenga kiwanja kipya nje ya Dar es Salaam ili kuangalia uwiano kwa lengo la kuishauri Serikali mapema zaidi kabla ya 2030.

Wabunge walilalamikia ukosefu wa ndege za kutoa huduma na zilizopo kutoza nauli kubwa wakati Serikali inaboresha zaidi miundombinu.

Mhandisi Sambali alieleza ukosefu wa ndege unatokana na ushindani wa kibiashara wa mashirika ya ndege ambapo mengine hayaji kwa kukosa abiria wanaounganisha safari za nje.

Pia alieleza Serikali kutokuwa na shirika imara la ndege kufuatia ATCL kuwa na ndege moja tu kumefanya asilimia 90 ya abiriawatumie nchi za jirani kuunganisha safari za nje.

Kufuatia maelezo hayo, wabunge waliitaka Serikali inunue ndege nne ili ATCL irudi hewani kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Magufuli.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani alisema wamepokea rai ya wabunge akisisitiza dhamira ya Serikali ni kununua ndege.

Uwanja wa Ndege wa Kigoma Kujengwa kwa Hadhi ya Kimataifa

Serikali imesema awamu ya pili ya Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma itaanza rasmi Julai mwaka huu.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema zabuni kwa ajili ya ujenzi zitatangazwa badae mwaka huu ili kuuwezesha Uwanja huo kuwa na hadhi ya kimataifa na kuchochea fursa za utalii katika ukanda wa Magharibi na Mwambao wa Ziwa Tanganyika.

Zaidi ya Shilingi Bilioni 40 kutoka Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB), zinatarajiwa kutumika hivyo kuwataka wananchi ambao eneo lao liko katika Uwanja huo kuondoka mara moja mara baada ya kulipwa fidia.

"Nia ya Serikali ni kuongeza njia ya kuruka na kutua ndege kutoka urefu wa mita 1800 sasa hadi mita 3100 na hivyo kuruhusu ndege kubwa aina ya Boeing 737 kutua katika uwanja huo", amesema Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amewataka wananchi wa Kigoma kutoa ushirikiano mkubwa kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege na Mamlaka ya Usafiri wa Anga ili zoezi la ujenzi lifanikiwe kwa haraka na kuepuka vikwazo vinavyoweza kuchelewesha mradi huo.

Naye Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe amewataka wananchi wa Kigoma na wawekezaji kujipanga kutumia fursa ya uwanja huo kuwekeza ili kukuza sekta ya utalii na usafirishaji katika Mwambao wa Ziwa Tanganyika pindi uwanja huo utakapokamilika.

"Tuna bahati kupata Serikali inayowekeza katika mkoa wa Kigoma, nawaomba wana Kigoma wenzangu tuepuke migogoro na kutumia fursa hii kuwekeza kikamilifu ili kukuza utalii katika ukanda wa Magharibi na kuongeza mapato katika mkoa wa Kigoma", amesisitiza Mhe. Zitto.

Amemhakikishia Profesa Mbarawa kuwa Uwanja wa Ndege wa Kigoma utafungua usafiri wa Anga kwa ukanda wa magharibi na nchi jirani na hivyo kuongeza idadi ya watalii na watumiaji wa usafiri wa anga katika mwambao wa Ziwa Tanganyika, hifadhi za Taifa za Gombe na Mahale na mikoa ya kanda ya magharibi.

Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Mkoani Kigoma Bw. Godlove Longole ameiomba Serikali kukamilisha Ujenzi wa uzio, Jengo la Abiria, Mnara wa kuongozea ndege na huduma za zimamoto katika uwanja huo ili kuuwezesha kufanya kazi zake kwa viwango vinavyotakiwa.

Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Kigoma Bw. Mohamedi Issa amemhakikishia Waziri kwamba atasimamia mchakato mzima wa mradi wa ujenzi kwa uadilifu, uaminifu ili thamani ya mradi huo iwiane na ubora wa kazi itakayofanywa na hivyo kuuwezesha uwanja huo kufikia kiwango cha Code 4C kinachowezesha ndege zenye ukubwa wa Boeing 737 kutua katika uwanja huo.

Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

UWEKAJI JIWE LA MSINGI LA MRADI WA UKARABATI NA UPANUZI WA KIWANJA CHA NDEGE CHA DODOMA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim M. Majaliwa, tarehe 20/07/2016 anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la mradi wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha ndege cha Dodoma.

Ukarabati huo utajumuisha urefushaji wa barabara ya kuruka na kutua ndege hadi kufikia urefu wa kilometa 2.5 kutoka Kilometa 2 za awali.

Kurefushwa kwa barabara hiyo, sasa kutatoa fursa kwa ndege kubwa Bombardier Q400, Gulfstream 550, ATR 72 n.k zenye uwezo wa kubeba abiria 90 kutua na kutumia uwanja huo.

Ukarabati huo unafanyika kwa fedha za Serikali ya Tanzania na unasimamiwa na Wahandisi wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA) kwa ushirikiano na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS).

Ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Dodoma ni miongoni mwa Miradi mbali mbali inayotekelezwa na Mamlaka ya viwanja Vya Ndege nchini kama vile Viwanja vya Tabora, Bukoba, Kigoma na Mwanza ambayo imekwisha anza na miradi mipya ya viwanja vya ndege vya Shinyanga na Sumbawanga itakayoanza hivi karibuni.


IMG 2183 IMG 2177 IMG 2183 IMG 2177

 

 

TAA kuanzisha Tuzo ya Utunzaji Mazingira kwa Viwanja Vya Ndege Nchini

image1Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) itatoa tuzo kwa viwanja vya ndege vitakavyofanya vizuri katika kutunza na kusimamia mazingira.

Hayo yalisemwa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Salim Msangi wakati wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania wakiadhimisha siku ya Mazingira Dunia kwa kufanya usafi nje ya kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam . TAA iliadhimisha Siku ya Mazingira Duniani kwa kufanya usafi (ambapo ilihusisha kyeka nyasi) na kuweka mbolea pamoja na kupunguza matawi ya miti iliyopandwa katika maadhimisho ya mwaka 2015.

Siku ya Mazingira Duniani itaadhimishwa kimataifa nchini Canada ikiongozwa na kaulimbiu ya "Connecting People to Nature", wakati kitaifa itafanyika mjini Butiama mkoani Mara ikiongozwa na kaulimbiu ya "Hifadhi ya Mazingira: Muhimili wa Tanzania ya Viwanda". Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa maadhimisho haya.

Msangi aliwataka meneja wa viwanja vya ndege vilivyo chini ya usimamizi wa TAA nchini kutunza mazingara, ambapo aliahidi TAA kutoatuzo kwa kiwanja kitakachofanya vizuri zaidi.

Alisema kuwa wafanyakazi wa viwanja vya ndege wamekuwa mstari wa mbele kutunza mazingira miaka yote ili kuhakikisha jamii inaishi katika eneo salama.

Mbali na kufanya usafi wa kufyeka nje ya Terminal 3, pia wafanyakazi hao, waliweka mbolea na kupalilia miti waliyopanda mwaka 2015 katika eneo la VIP na pembeni mwa barabara ya kuelekea Kago (Cargo) . Vilevile matawi ya baadhi ya miti yalipunguzwa.

Kila mwaka wafanyakazi hao wa TAA wamekuwa wakishiriki katika maadhimisho hayo muhimu kwa kufanya shughuli mbalimbali kamavile kupanda miti, kufanya usafi n.k. katika maeneo tofauti tofauti.

Akifafanua kuhusu tuzo, Msangi alisema kuwa TAA itaanzisha tuzo ya kuhifadhi na kusimamia Mazingira (DG Environmental Award) na atakayeshinda atapewa tuzo hiyo itakayoshindaniwa na viwanja vyote vilivyo chini ya usimamizi wa TAA.

"Itaanzishwa tuzo na kiwanja kitakachoshinda, meneja wakiwanja hicho pamoja na wafanyakazi husika watazawadiwa tuzo na TAA ili kuhamasisha viwanja vingie navyo vifanye vizuri na kushinda kwenye maadhimisho yanayokuja, "alisema Msangi.

Kaimu Mkurugenzi wa TAA pia alizitaja shughuli zingine zinazofanywa na Mamlaka ili kutunza mazingira ni pamoja na kudhibiti maji taka yanayotoka viwajani, ambapo kuna mabwawa (oxidation ponds) yanayokusanya majitaka yote na kuyasafisha ili kukidhi viwango vilivyowekwa.

Mbali na kusafisha majitaka pia kuna mfumo (oil separator) wa kutenganisha maji na mafuta ili kulinda mazingira. Maji ya mvua yote yanayotoka katika eneo la maengesho ya ndege yameelekezwa katika mfumo huu ili kutenganisha maji na mafuta kabla ya kuyaruhusu kwenda kwenye mazingira.

Kupanda miti imekuwa ikipendezesha maneo na pia ikipunguza mrundikano wa gesi ukaa again, ambapo usafiri wa anga umekuwa ukichangia takribani 2% ya gesi ukaa (CO2) inayozalishwa dunia.

image2Mkuu wa Kitengo cha Mazingira, Jofta Timanywa alisema kuwa kila mwaka TAA imekuwa ikiadhimisha siku Siku ya Mazingira Duniani kwa kufanya kazi mbalimbali za kuhifadhi na kusimamia mazingira ikiwemo usafi maeneo mbalimbali pamoja na kupanda miti. 

 

 

 


image3

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Salim Msangi (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa TAA, Mohamed Ally wakifanya usafi nje ya jengo la kuwasili na kuondokea abiria mashuhuri (VIP) leo wakati wafanyakazi wa mamlaka hiyo wakiadhimisha Siku ya Mazingira.

image4

Wafanyakazi wa TAA wakifanya usafi leo katika eneo la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (Terminal III)

image5

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) baada ya kumaliza kufanya usafi nje ya Kwanja wa Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) leo.

 

Taasisi Zilizochini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Zaadhimisha Siku ya Mazingira Duniani kwa Kufanya Usafi Mabibo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia namna samaki anaweza kufugwa vizuri bila kuharibu mazingira na kuleta manufaa kabla ya kuhutubia kwenye kilele cha siku ya mazingira duniani kwenye viwanja vya Mwenge,Butiama.Siku ya Mazingira Duniani huadhimishwa tarehe 05 mwezi Juni kila mwaka, ikiwa na lengo kuhamasisha jamii duniani kote kuelewa masuala yahusuyo Mazingira na pia kuhamasisha watu wa jamii mbalimbali duniani kuwa mstari wa mbele katika kuchukua hatua za kuhifadhi na kulinda mazingira.

Kwa mwaka 2017, maadhimisho haya kimataifa yalifanyika nchini Canada yakiongozwa na kaulimbiu ya "Connecting People to Nature" (yaani mahusiano endelevu kati ya binadamu na mazingira). Kitaifa Siku ya Mazingira Duniani ilifanyika Mjini Butiama ikiongozwa na Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Hifadhi ya Mazingira: Muhimili wa Tanzania ya Viwanda". Kaulimbiu hii inahamasisha wananchi kuwa na urafiki enedelevu na mazingira asilia ambapo kila mtu anapaswa kutambua, kufurahi, kujivunia na kulinda uzuri wa mazingira asilia yetu na kuhamasishana kuyatunza na kuhifadhi.

Kitaifa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Dunia yalifanyika katika Uwanja wa Mwenge Mjini Butiama ambapo pamoja na sherehe hiyo kulikuwapo na Kongamano na shughuli mbalimbali kuhusiana na masuala ya Mazingira ambapo jumla ya miche ya asili 1,500 ilipandwa katika maeneo mbalimbali ya mji wa Butiama.

Aidha, katika zoezi hili Serikali inategemea kuwapo kwa faida zifuatazo:-

 1. Kuijengea jamii uwezo juu ya uelewa wa masuala ya mazingira na changamoto za kijamii zinazojitokeza katika utunzaji wa Mazingira.
 2. Kuwawezesha wadau kushiriki katika fursa zinazohusiana na upandaji wa miti.
 3. Kujadili mwendelezo wa utekelezaji wa shughuli zilizoratibiwa katika Mkoa na Wizara kuhusu namna bora ya uhifadhi wa Mazingira.
 4. Kuelemisha wananchi kupanda miti ili kukidhi mahitaji ya Dunia kupambana na ongezeko la hewa ya Carbon dioxide (Ukaa).
 5. Kuenzi kazi zote za Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere katika hifadhi ya mazingira.

Maadhimisho katika Ngazi ya Wizara
Sekta ya Uchukuzi katika Wizara Ya Ujenzi,uchukuzi Na Mawasiliano imekuwa kila mwaka ikishiriki katika maadhimisho ya Siku ya Mazigira Duniani kwa kufanya shughuli mbalimbali. Mwaka huu Sekta ya Uchukuzi pamoja na taasisis zake iliungana na sekta nyingine nchini katika kuadhimisha siku ya mazingira Dniani Sekta ya uchukuzi iliadhimisha siku hii muhimu kwa kufanyakazi mbalimbali ikiwa pamoja na kupima utaoaji wa gesi joto kutoka kwenye Magari, Kupanda miti kufanya usafi katika maeneo ya Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) pamoja na maeneo ya jirani.

image2Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dk. Leonard Chamuriho aliyekuwa Mgeni rasmi akiwahutubia wafanyakazi wa taasisi zilizopo chini ya sekta hiyo, kabla ya kuanza kwa zoezi la kufanya usafi wa mazingira kwenye Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) na Soko la Mabibo, ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani iliyoadhimishwa jana.

 Awali kabla ya kuanza kwa usafi huo, Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi, Dr. Leonard Chamuriho aliyekuwa mgeni rasmi alisema, Jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine nchini limeendelea kuathirika na uchafunzi wa mazingira kwa njia mbalimbali, ambapo amewataka wafanyakazi kufanya usafi wa mara kwa mara.

Dr. Chamuriho alisema usafi wa mazingira unaondoa na kuzuia magonjwa ya milipuko yanayosababishwa na uchafu, endapo mazingira hayatasafishwa ipasavyo.

Hata hivyo, alisema usafi uendane na Kaulimbiu ya Siku ya Mazingira Kimataifa ya Mahusiano Endelevu kati ya Binadamu na Mazingira, wakati ya Kitaifa ni Hifadhi ya Mazingira Muhimili kwa Tanzania ya Viwanda.

"Tunaungana na wenzetu kusafisha mazingira lakini pia tujenge tabia ya kufanya usafi wa mara kwa mara, ili kujilinda na magonjwa ya milipuko," alisema Dr. Chamuriho.

Mbali na kupanda miti na kusafisha mazingira pia sekta ilifanya upimaji wa kiwango cha gesi toka kwenye magari.


image3

Mkuu wa chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) Mhandisi. Profesa Zacharia Mganilwa (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dk. Leonard Chamuriho (wapili kutoka kushoto), Mwenyekiti Serikali za Mtaa wa Mabibo (wapili kutoka kulia) na Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege vya Mikoa (DRA) kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Ndugu Valentine Kadeha (wakwanza kulia) wakiwawanaelekea kwenye soko la Mabibo kufanya usafi.

image4

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dk. Leonard Chamuriho akishiriki zoezi la usafi katika Soko la Mabibo pamoja na wafanyakazi kutoka taasisi mbali mbali zilizo chini ya wizara yake

image5

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dr. Leonard Chamuriho akipanda mti ndani ya Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT), ikiwa ni moja ya kazi zilizofanyika jana kwenye kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, iliadhimishwa kwa kufanyika usafi maeneo ya nje ya chuo hicho na soko la Mabibo.

image6

Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege vya Mikoa (DRA), Bw. Valentine Kadeha (katikati) akishirikiana kupanda mti na wanafunzi wa shule ya Mpakani ya Mabibo, katika maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, iliyoadhimishwa jana kwa wafanyakazi wa taasisi mbalimbali wa Sekta ya Uchukuzi kufanya usafi nje ya Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) na Soko la Mabibo.

image7

Mojawapo wa Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Swalha R. Soka akishiriki zoezi la upandaji miti ndani ya Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT)

image8

Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mpakani akishiriki zoezi la upandaji miti katika maadhimiso ya siku ya mazingira duniani.

image9

Mmoja wa wafanyakazi wa Chuo cha Usafirishaji akiwa anaeleza kwa mgeni rasmi madhara ya gesi ya ukaa inayotokana na magari na namna chuo hicho kinavyoweza kupima magari na kutoa ushauri kwa watanzania katika kukabiliana na matatizo ya kimazingira yanasosababishwa na gesi ya ukaa.

image10

Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mpakani mara baada ya kumaliza zoezi la usafi wa mazingira.

 

 

VIP TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

EXTENSION OF TENDER OPENING FOR SUPPLY OF FIRE TENDERS

EXTENSION OF TENDER OPENING FOR SUPPLY OF FIRE TENDERS NOV 23 2017-1

Wakwepa kodi marufuku TBIII – Mhe. Naibu Waziri Eng.Nditiye

WAFANYABIASHARA wenye kulipa kodi na kuingizia serikali mapato kwa wakati ndio watakaopata nafasi ya kuwekeza kwenye jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), imeelezwa.

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye alipofanya ziara ya kutembelea Makao Makuu ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na kumalizia TBIII.

Mhandisi Nditiye amesema baada ya kukamilika kwa jengo hilo baadaye mwakani, wafanyabiashara watakaopewa kupaumbele hususan waliopo kwenye Jengo la zamani (TBI) na jengo la pili (TBII) ni wale tu wanaozingatia ulipaji wa kodi na mapato yote ya serikali kwa wakati.

"Tunajua wapo wengi waliojitokeza kuomba maeneo ya kufanya biashara, lakini wale ambao watahama kutoka majengo yetu haya mawili la TB I na TBII tunawaambia wazi kabisa kuwa wale waaminifu na waadilifu wenye kulipa kodi ya pango na mapato mengine ya serikali kwa wakati ndio wanafikiriwa kwanza, na wale wasiolipa kwa wakati hawatapewa nafasi kabisa ya kuwekeza kwenye jengo hili," amesisitiza Mhe. Nditiye.

Hata hivyo, Mhe. Nditiye amesema tayari ameuagiza uongozi wa TAA kuhakikisha wanapitia mikataba yote ya biashara kwenye majengo hayo ya abiria na kutengeneza upya ile yenye matatizo ili iweze kuleta tija kwa taifa, kwani kwa sasa kumekuwa na mikataba ya hovyo.

Amesema TBIII inafursa za biashara ambapo inaeneo kubwa la kujenga hoteli, migahawa na sehemu za kupumzikia watu, hivyo kuwataka wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza.

"Juzi tu nilikutana na Wajerumani nikawaeleza tunaeneo la uwekezaji hapa TBIII na kule Msalato mnapotarajia kujenga kiwanja cha kimataifa, na wameonesha nia ya kuja kuwekeza, nia ya serikali na tupo pamoja katika uwekezaji wa maeneo yetu mbalimbali, ili kujiimarisha katika uchumi," amesema Mhandisi Nditiye.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela amesema kuwa wanatarajia watoa huduma na wafanyabiashara watakaokidhi vigezo na masharti ya kutoa huduma bora ndio wakaopata nafasi kwenye jengo hilo la tatu.

"Pia tunatarajia watoa huduma na wafanyabiashara ni wale wanaokodhi vigezo kwa hiyo yote yanalenga katika kuhudumia watanzania na kukuza sekta ya usafiri wa anga na kuhudumia vizuri wale wanaopita hapa," amesema Bw. Mayongela.

Amesema jengo hilo likikamilika litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria takribani milioni sita (6) kwa mwaka ambalo ni ongezeko kubwa ukilinganisha na jengo la sasa la TBII linauwezo wa kuihudumia kati ya abiria milioni 1.2 hadi 1.5 kwa mwaka.

Hivyo tunaishukuru serikali kwa kutupa ushirikiano katika kuendeleza viwanja vya ndege, pia kwa upande wa TAA wamekuwa wakifanya matengenezo madogo madogo kwa kutumia fedha za bajeti ya ndani.

Hivi karibuni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa ameitaka TAA kuwaondoa wafanyabiashara wote wasiolipa kodi na mapato mengine ya serikali kwa wakati, kutokana na kukwamisha juhudi za serikali za ukusanyaji mapato.

ADVERT OF TENDER FOR CAR PARK, JNIA, MWANZA AND ARUSHA

Welcome to TAA

Tanzania Airports Authority (TAA)  was established on 29th November 1999 vide Government Notice Number 404 of 1999 under the Executive Agency Act Number 30 of 1997. The Authority assumed the functions of the former Directorate of Aerodromes under the Ministry of Communications and Transport currently the Ministry of Transport. The establishment of the Agency is part of the Government efforts in changing the public service structure which is geared towards improving service delivery

Latest News

Contact Us

Tel (Gen): +255 22 2842402/3
Fax: +255 22 2844495
Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
P.O.Box 18000 Dar Es Salaam

Social Sites & Blog

Feedback & Enquires